Kuna jamaa alifungwa jela miaka 7 kwa kosa la wizi wa mamilioni ya pesa. Baada ya miaka 2 akiwa jela anapata barua toka kwa babake

"Mwanangu mpendwa umeniacha Katika hali ya uzee na maradhi, wakati wa kutayarisha shamba umefika, na sina mtu wa kunilimia, natamani ungekuwepo ukanisaidia kulima na kupanda mahindi. Tutaonana mungu akipenda. Mtoto akajibu- Baba tafadhali usije lima katika hilo shamba kwa sasa mpaka nitoke jela, pesa zote nilizoiba nimezifukia Katika shamba hilo. Kwa kuwa barua zote za wafungwa husomwa na Askari wa gerezani. Baba siku ya pili alipoamka akakuta Askari magereza zaidi ya 100 wanalima shamba. Mpaka wakamaliza wasipate kitu. Mtoto akamwandikia Baba yake, Mpendwa baba natumai msaada niliokupa umeufurahia, panda mahindi sasa.